Wafuasi wa Spika Elachi na Gavana Sonko wazozana bungeni

Vita vya ubabe katika bunge la kaunti ya Nairobi vinazidi kushamiri kila uchao. Leo spika wa bunge hilo Beatrice Elachi, ameapa kutomkubali Jacob Ngwele kama karani wa bunge hilo miezi kadhaa baada ya kutimuliwa afisini mwake kwa tuhuma za kuwa hakuajiriwa kupitia njia halali. Spika Elachi aliandika barua kwa tume ya kupambana na ufisadi akitaka ngwele achunguzwe lakini hilo halijatimia. Elachi anashikilia kwamba Edward Gichana ndiye karani wa bunge hilo.

Read More
From: Kenya CitizenTV

Back to Home