Mtu mmoja atafunwa na kiboko hadi kufa huko Lonkwar Samburu

Mtu mmoja atafunwa na kiboko hadi kufa huko Lonkwar Samburu

Mwanamume mmoja ameuawa baada ya kuvamiwa na kiboko katika kijiji cha Lonkwar kaunti ya Samburu.
Akithibitisha kisa hicho, naibu kamanda wa polisi katika kaunti ndogo ya Samburu ya kati Abdikadir Malicha,amesema muathiriwa alikuwa anatembea kutoka kijiji cha Lonkwar kuelekea kijiji jirani alipovamiwa na mnyama huyo saa tatu usiku. Malicha amewahimiza wakazi kuwa wangalifu zaidi na kuripoti mnyama yeyote hatari atakayeonekana karibu na makazi ya watu kwa kituo cha polisi kilicho karibu au hata afisi za shirika la KWS ili hatua zichukuliwe kuzuia mashambulizi ya wanyamapori dhidi ya binadamu. Wakazi wanasema kuwa kiboko huyo amekuwa akionekana katika kijiji hicho kwa muda wa siku tatu kabla ya kumvamia marehemu.

Read More
From: Kenya CitizenTV

Back to Home