Mtoto aliyeibwa kutoka nyumbani huko Misikhu bado hajapatina

Mtoto wa mwaka mmoja na miezi kumi aliyeibiwa wiki iliyopita katika eneo la misikhu kaunti ya bungoma bado hajapatikana.
Kisa hicho kilitokea wakati mamake mtoto huyo alipokuwa ameenda kutafuta maziwa asubuhi ili aaendae staftahi. Mamake mtoto huyo auma anyoso ameiambia runinga ya citizen kuwa alimwacha mwanawe kitandani na kutoka nyumbani kwenda dukani lakini aliporejea mwanawe alikuwa ametoweka. Babake mtoto huyo anasema kuwa matapeli wameanza kuitisha familia hiyo fedha wakidai wanamzuilia mtoto wao mchanga. Kisa hicho kimethibitishwa na naibu wa chifu wa eneo hilo aliyewataka wazazi kutoa taarifa zozote kumhusu mtoto huyo kwa polisi.

Read More
From: Kenya CitizenTV

Back to Home