Magavana wadai kucheleweshwa kwa ugavi wa fedha kumeathiri shughuli

Kucheleweshwa kwa ugavi wa fedha za bajeti ya mwaka 2019/20 huenda ndio chanzo cha serikali za kaunti kushindwa kujiandaa katika vita dhidi ya virusi vya corona. Haya ni kwa mujibu wa ripoti ya baraza la magavana katika kikao cha saba tangu mfumo wa ugatuzi kuanza humu nchini. Aidha magavana wanasema huduma za afya huenda zikaathirika zaidi kwa sababu ya idadi ndogo ya wahudumu wa afya katika kaunti. Hata hivyo wamepongeza ugatuzi wakisema umeleta maendeleo katika kaunti mbali mbali ila uhusiano baina ya serikali kuu na zile za kaunti unapasa kuimarishwa zaidi.

Read More
From: Kenya CitizenTV

Back to Home