Maafisa watatu wa polisi wajeruhiwa kwenye shambulio katika kituo cha polisi cha hagadera

Maafisa watatu wa polisi wanaendelea kuuguza majeraha kufuatia shambulizi la bomu la wapiganaji wa Alshabaab katika kambi ya polisi ya Yumbis kaunti ya Garissa.
Tukio hilo lilitokea jana mwendo wa saa moja jioni. Maafisa hao walishambuliwa kwa risasi na kujeruhiwa wakati wa makabiliano hayo. Afisa John Njenga alipata majeraha ya mguu na mkono, huku Afisa Abraham Musombi akijeruhiwa kwenye mkono wa kulia naye Dennis Musyoka akipata jeraha la risasi kwenye paja. Baada ya shambulio hilo, maafisa hao walipelekwa kwa matibabu ya dharura katika hospitali ya Hagadera kabla ya kusafirishwa hadi hospitali ya rufaa ya Garissa ambapo wanaendelea kupokea matibabu.

Read More
From: Kenya CitizenTV

Back to Home