Hazina ya dharura ya COVID-19 yatoa vifaa kwa hospitali ya rufaa ya Kitale

Hazina ya dharura ya kupambana na janga la corona kwa ushirikiano na wakfu wa benki ya equity leo Imezuru kaunti ya Trans Nzoia ambapo imetoa vifaa vya matibabu kwa hospitali ya rufaa ya Kitale.
Vifaa hivyo vinavyojumuisha magwanda ya hospitali na maski vinakusidiwa kuwasaidia wahudumu wa afya wakati huu ambapo taifa linakabiliana na ongezeko la maambukizi ya virusi vya corona. Afisa mkuu wa benki ya Equity Polycup Igathe ametaka bunge la kaunti hiyo kuwatengea madaktari na wauguzi fedha za kutosha ili kuhakikisha wanafaulu katika vita dhidhi ya janga hili. Naye Gavana Patrick Khaemba amewataka wakazi kuwa makini na kufuata maagizo yaliyotolewa na serikali kujilinda na corona.

Read More
From: Kenya CitizenTV

Back to Home